SHAMBA LA CHUMVI LANAWIRI TENA
Ilikuwa ni Muda ambao Ndoto ya mpwani kuimarika ilititiliwa kikomo kusawazisha mahangaiko,maisha duni,Uhuni na hali zisizoeleweka Kwa ujumla. Bandari ya mombasa ni moja ya kitega uchumi eneo bunge hilo na hata taifa zima la kenya na hii imekuwa faida kuu kwa wakaazi eneo bunge hilo ambao wamenawiri kupata ajira na kupanua biashara zao kwa kipindi cha miaka mingi. Kwenye serikali iliyotoka mamlakani mambo hayakuwa sawa kwa mpwani kwa amri iliyotolewa ya uhamisho wa almashauri ya bandari kutoka mombasa Hadi naivasha Kwa misingi isiyopo na Majibu .Kulingana na Wengi waliitamka kama dhulma ya kuwafaidi matajiri na kuwaponza maskini .Hili lilizua mchepuko mkubwa Kwa wakaazi kwani walihisi kutolewa Tonge mdomoni. Waajiriwa wengi wakakosa nafasi za kazi kwa kuwepo sheria ya usafiri wa shehena ya mizigo kupitia reli kinyume na vile Ilikuwa kama zamani pale lorry la trela lilitumika kufanya shuhuli hii.maderava Wengi Unga Wao ukamwagika . Kampuni nyingi Ambazo ziliitegemea bandari hii kwen...