Posts

Showing posts from November, 2022

MAWINGU YA LAANA

Image
Mara nyingi tunafahamu fika mawingu yakitanda angani huwa ni mvua ipo tayari kunyea ishara ya baraka lakini hili limegeuka kinaya!. kwa zaidi ya misimu minne ardhi yetu imekuwa ikishuhudia kiangazi kikali kisichodhibitika kwa hali ya kushangaza au labda tuseme mkosi mbaya .      picha kwa hisani ya gazeti la star Kulingana na utafiti wa wanasayansi limetajwa swala la kuchafuka kwa anga kwa mambo tunayoyafanya sisi binadamu ikiwemo utumizi wa kemikali sumu,ukataji miti na uchafuzi wa mazingira na mengineo mambo yanayosababisha kuvuja kwa miale mikali ya jua inayopasua ardhi na kuiacha nchi kavu. .    Picha kwa hisani ya gazeti la star  Hapa nchini zipo sehemu zenye hatari hii kubwa ikiwemo ; Garissa, Isiolo, Kajiado, Kitui, Mandera, Marsabit, Laikipia, Samburu, Tana River, Turkana, na wajir .    Picha kwa hisani ya gazeti la star   Utafiti umebaini kuwa zaidi ya raia milioni nne nukta moja wanaoishi kwe...