VIJANA KAZINI
. Picha ya vijana mombasa Je, vijana ni kina Nani...? ,wengi huwazungumzia kwa kauli bora ya uongozi wa kesho wenye maarifa na Nguvu zaidi kwenye milki ya majukumu mazito Sio tu ya familia bali ya jamii nzima. Kwa kipindi cha muda mrefu hapa nchini wimbo wa ukosefu wa ajira umekuwa kama kibwagizo kila kuchao huku maelfu ya wanafunzi wanaohitimu vyuoni wakibanana mjini kila mmoja akiwa na lengo la kufanikisha maisha. Licha ya msururu huu wa neno "Sina Kazi " kusambaza kwa kasi, vijana wameweza kufunguka macho na kuona ya mbeleni huku wakizamia kwenye mitandao ili kukwachua vibarua vya peni kadhaa kwa kimombo tunaziita "online jobs". . Picha kwa hisani ya Ajira Wengine wamejitosa kwenye mashirika kadhaa yanayotoa mafunzo ya kiufundi, ufadhili wa miradi na biashara aidhaa kwa vikundi au mtu binafsi maswala yanayompa kijana uwanja wa kujiendeleza. . picha kwa hisani ya shirika la Swahili ...