MSIMAMO WA VOICE OF MOMBASA
. kundi la vugu vugu mombasa . picha ya michael nato akizungumza Kundi la (voice of mombasa) alamaarufu vugu vugu mombasa pamoja na wananchi Katika mahojiano yamoja kwa moja na wanahabari wamepitisha ujumbe kwa Rais Daktari William Ruto kuweza kutangamana nao atakapokuwa akidhuru mombasa. . picha ya michael nato akizungumza Msemaji wao mkuu Bwana Michael Nato amemrai rais huku akimtaka atenge muda wa mazungumzo kwa viongozi waliowaniwa viti vya udiwani kwenye chama cha UDA ila hawakufua dafu. Malengo Yao na madhumni yakiwa kutimiziwa ahadi walizoahidiwa na rais wakati wa kampeni. . Picha ya Elizabeth kadzo akihutubia Pia, kundi hili limeweza Kuonyesha kughadhabishwa mno na tukio la vurugu lililotokea GTI hapa mombasa mnamo mwezi uliopita kwenye mkutano mkubwa wa UDA uliongozwa na karani mkuu bwana CLEOPHAS MALALA. ...