HOSSANA AJIPANGA VIKALI DHIDI AHARUB SUPER CUP


   (Picha ya Hossana akipepeta mpira)
Diwani wa wadi ya chaani eneobunge la changamwe - Mombasa, Franklin Hossana makanga aliteua  timu ya chaani FC combined kupitia michuano ya kirafiki ili kuwakilisha wadi hiyo kwenye  ligi ya Aharub Super Cup.

  (Picha ya Hossana Pamoja na wachezaji       Kabla Mchuano )
Michuano hiyo ilishirikisha timu hatari ambazo ni Blue Rangers FC, chaani youth na wazito FC ,timu ambazo zilimenyana ili kupata wachezaji bora ambao waliijumuishwa kuwa kikosi kimoja cha wadi hiyo .

Aharub Super Cup ,ni ligi inayopangiwa kuanza mnamo tarehe tisa mwezi ujao na kuchezwa kwa miezi miwili mfulululizo Hadi kumalizika.Ligi hii itashirikisha  wadi zote katika kaunti ya mombasa kwenye michuano mikali kwa mathumni ya kuinua talanta mashinani na kuwawezesha wachezaji  kupata fursa ya kung'aa.

.   ( Picha ya wazito fc)
Timu hizi za wadi, zimewekwa kwa makundi pale timu ya chaani ward combined wapo kundi la D pale watamenyana na wadi ya mtongwe, Tononoka na mikindani.Baada ya hapo,wataweza kuingia kwenye kumi na sita bora , kisha quarter fainali,semi fainali na mwishowe fainali pale kuna zawadi kuu ya kushindaniwa.

Chaani FC combined wapo ngangari kushiriki ligi hii pale Hosanna amewapa majezi ya kutosha pia kuwapa mkufunzi ambaye atawanoa makali kwenye mazoezi yanayoanza hii wiki.

.   ( Picha ya chaani FC combined )
Pia ,Hossana aliwasihi vijana kufunguka macho na kuona nafasi kuu maishani haswa kuweza kutangamana na wachezaji wengine pamoja na kuwataka wazingatie bidii na  nidhamu  ili kutwaa taji hilo.

Akizidi kuzungumza, Hossana  alitaja uwanja wa chaani kuwa ameufanyia mchakato uweze kutengezwa kama stadium ndogo kwa malengo ya kuinua soka kwenye wadi hiyo.
"Nimewasilisha ombi katika bunge la kaunti ili waweze kutengeza uwanja huu wa chaani kuwa kama stadium ndogo pale utawezesha sok kwenye wadi hii ya chaani" Alisema .
Mwisho .

© AKILINYINGI MEDIA
      MOMBASA 



Comments

  1. Hali halisi,Ukweli mtupu, Wapinzani wataona vumbi

    ReplyDelete
  2. I wish all the best Team chaani

    ReplyDelete
  3. Sote mbele pamoja

    Tunaomba team ya wamama fc piaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

    ReplyDelete
  4. All the best team chaani...kudos Hossana i believe in you doc

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VIJANA KAZINI

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.