HOSSANA AJIPANGA VIKALI DHIDI AHARUB SUPER CUP
Diwani wa wadi ya chaani eneobunge la changamwe - Mombasa, Franklin Hossana makanga aliteua timu ya chaani FC combined kupitia michuano ya kirafiki ili kuwakilisha wadi hiyo kwenye ligi ya Aharub Super Cup.
Michuano hiyo ilishirikisha timu hatari ambazo ni Blue Rangers FC, chaani youth na wazito FC ,timu ambazo zilimenyana ili kupata wachezaji bora ambao waliijumuishwa kuwa kikosi kimoja cha wadi hiyo .
Aharub Super Cup ,ni ligi inayopangiwa kuanza mnamo tarehe tisa mwezi ujao na kuchezwa kwa miezi miwili mfulululizo Hadi kumalizika.Ligi hii itashirikisha wadi zote katika kaunti ya mombasa kwenye michuano mikali kwa mathumni ya kuinua talanta mashinani na kuwawezesha wachezaji kupata fursa ya kung'aa.
Timu hizi za wadi, zimewekwa kwa makundi pale timu ya chaani ward combined wapo kundi la D pale watamenyana na wadi ya mtongwe, Tononoka na mikindani.Baada ya hapo,wataweza kuingia kwenye kumi na sita bora , kisha quarter fainali,semi fainali na mwishowe fainali pale kuna zawadi kuu ya kushindaniwa.
Chaani FC combined wapo ngangari kushiriki ligi hii pale Hosanna amewapa majezi ya kutosha pia kuwapa mkufunzi ambaye atawanoa makali kwenye mazoezi yanayoanza hii wiki.
Pia ,Hossana aliwasihi vijana kufunguka macho na kuona nafasi kuu maishani haswa kuweza kutangamana na wachezaji wengine pamoja na kuwataka wazingatie bidii na nidhamu ili kutwaa taji hilo.
Akizidi kuzungumza, Hossana alitaja uwanja wa chaani kuwa ameufanyia mchakato uweze kutengezwa kama stadium ndogo kwa malengo ya kuinua soka kwenye wadi hiyo.
"Nimewasilisha ombi katika bunge la kaunti ili waweze kutengeza uwanja huu wa chaani kuwa kama stadium ndogo pale utawezesha sok kwenye wadi hii ya chaani" Alisema .
Mwisho .
© AKILINYINGI MEDIA
MOMBASA
Great article ππ
ReplyDeleteHali halisi,Ukweli mtupu, Wapinzani wataona vumbi
ReplyDeleteI wish all the best Team chaani
ReplyDeleteSote mbele pamoja
ReplyDeleteTunaomba team ya wamama fc piaπππ
All the best team chaani...kudos Hossana i believe in you doc
ReplyDelete