SHAMBA LA CHUMVI LANAWIRI TENA

Ilikuwa ni Muda ambao Ndoto ya mpwani kuimarika ilititiliwa kikomo kusawazisha mahangaiko,maisha duni,Uhuni na hali zisizoeleweka Kwa ujumla.

Bandari ya mombasa ni moja ya kitega uchumi eneo bunge hilo na hata taifa zima la kenya na hii imekuwa faida kuu kwa wakaazi eneo bunge hilo ambao wamenawiri kupata ajira na kupanua biashara zao kwa kipindi cha miaka mingi.

Kwenye serikali iliyotoka mamlakani mambo hayakuwa sawa kwa mpwani kwa amri iliyotolewa ya uhamisho wa almashauri ya bandari kutoka mombasa Hadi naivasha Kwa misingi isiyopo na Majibu .Kulingana na Wengi waliitamka kama dhulma ya kuwafaidi matajiri na kuwaponza maskini .Hili lilizua mchepuko mkubwa  Kwa wakaazi kwani walihisi kutolewa Tonge mdomoni.

Waajiriwa wengi wakakosa nafasi za kazi kwa kuwepo sheria ya usafiri wa shehena ya mizigo kupitia reli kinyume na vile Ilikuwa kama zamani pale lorry la trela lilitumika kufanya shuhuli hii.maderava Wengi Unga Wao ukamwagika .

Kampuni nyingi Ambazo ziliitegemea bandari hii kwenye Njia ya kusafirisha shehena zikashindwa kupata nafasi ya kupenya kirahisi na kupunguza wafanyikazi wao kwa madai ya upungufu wa kazi.

Janga hili likawa linamkumba kila raia anayeishi eneo bunge hilo kwa njia moja au nyingine.Nafkiri hata mama muuza chakula pale wateja wake wanapokosa Kazi pia yeye hukosa Kazi hili linaeleweka.

Mgomo wa kila mara kupitia mashirika ya haki ikiwemo "Haki Afrika" ukawa unashuhudiwa huku wakaazi wakiwa na Ombi Moja la kurudisha madereva kazi  swala ambalo liligonga vichwa vya habari na Sululu Ikawa vigumu kupatikana.

Kwenye muda wa kampeni ndipo kizaazaa kilianza kuchipuka pale waheshimiwa walitumia Swala la uhamisho Wa bandari kama sera za kumuuzia mpwani Ili wazoe kura nyingi.Nao wapwani wakawa mwamba mgumu kwa walichikiona Hapo nyuma .

Baada ya uchaguzi ndipo Rais Wa Tano Wa jamuhuri ya Kenya alipotoa Amri na pia Kutimiza sera Yake Kwa mpwani . Shuhuli za bandari Kurudi kama ilivyokuwa zamani . Mwanga umeweza Kurudi tena Kaunti hii ya Mombasa . 

Akilinyingi.
Mombasa.

Comments

  1. Mwanga umerudi bandari angalau watu wa pwani wapate riziki. ..

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri bro.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Ama kweli. Umelifufua jambo
    Kazi safi kaka

    ReplyDelete
  5. Good job ๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  6. Kazi safi #AKILINYINGI

    ReplyDelete
  7. ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ฏ

    ReplyDelete
  8. Kazi nzuri,lakin rekebisha Tu makosa kidogo,Mombasa ni gatuzi si eneobunge, usichanganye lugha mbili mf.Lorry tumia Kiswahili sanifu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VIJANA KAZINI

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.