MASTAR WA DESTINY WASHINDA KWENYE CHANGAMWE TALENT SEARCH



   Picha vijana Wa destiny wakipewa kombe

Yamekuwa ni mashindano Makali yaliyoandaliwa na Mbunge wa Changamwe Mheshimiwa Omar Mwinyi Shimbwa lengo likiwa ni kuinua Sanaa na kuwaleta Pamoja walio na talanta Tofauti Ili kuwatambua  na kuwapa fursa wenye vipaji kwenye eneo bunge hilo.

Changamwe Talent Search ilitangulizwa na mchujo kwenye wadi tofauti ikiwemo: Changamwe,Chaani ,Kipevu, Airport na Portritze ambapo washindi wawili Kila wadi waliteuliwa kwenye fainali  kumenyana na wenzao  bomu stadium.

Mazoezi yamekuwa ya uangalifu mno pale waandalizi wakuu walishirikiana na vitengo tofauti Vya Sanaa :Kusakata ,kuigiza ,Shairi ,na Kuimba Ili kuhakikisha Kila mwaniaji Yupo kwenye Njia sawa na atazifwata sheria zinazostahili


.     picha ya vijana wa kundi destiny 

Vijana Wa destiny international home of Talents Muda Huu Wamekuwa wakitia Bidii kwenye mazoezi huku wakijuwa mtaka Cha mvunguni sharti ainame.Wamekuwa wakinoa Makali kwenye Kusakata densi ,uigizaji na Shairi vitengo ambavyo Wamekuwa na umakinifu navyo.


    Picha vijana wa destiny wakisakata

Kwenye fainali ni maajabu yamefanywa hapa ndipo wale wasanii ibuka wamechana mistari kuwaacha mashabiki Kwa shangwe  na mshangao. Vijana Wa destiny walifunika Zaidi Kwa vitengo vyao na kujizolea vikombe vitatu ,vyeti vitatu na elfu Kumi na tisa Pesa taslimu .kundi ambalo lilizoa zawadi nyingi na Kuwa mshindi Mkuu Kwa jumla.

.   Picha Vijana Wa destiny wakifurahia     ushindi

#Akilinyingi.
#fikrazakichawi.
#Mombasa.

Comments

Popular posts from this blog

VIJANA KAZINI

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.