BARUA KWA RAIS
Kundi la VUGU VUGU mombasa likiongozwa na msemaji mkuu bwana Michael Nato ambaye aliwania kiti Cha udiwani katika wadi ya chaani -changamwe pamoja na viongozi wengine,wamehutubia wanahabari kwa malengo yakumfikishia Rais William Ruto matakwa yao yanayohusu mgao wa nyadhifa katika serikali.
Bwana Michael Nato akizungumza, amepongeza juhudi anazozifanya Rais kwa kusema kuwa anazidi kuafikia malengo alioahidi wakenya kipindi cha kampeni .
Pia, amemsihi Rais kuweza kuwakumbuka viongozi waliokosa kufua dafu kwenye kinyang'anyiro cha kampeni mwaka uliopita hii ni ikiwemo madiwani waliowania katika kiti cha UDA ,Bwana Isaac Malila aliyewania kiti cha ubunge Changamwe, Bi. Selina Maithya aliyekuwa mpenzi mwenza (Running mate) w aliyewania kiti cha gavana mombasa ambaye kwa sasa ni mbunge wa afrika mashariki Hassan Sarai Ili atimize kama walivyokuwa wameagana kipindi cha kampeni.
Amemtaja karani mkuu wa chama cha UDA bwana Cleophas Malala kama mchapa kazi na kumuomba kuweza kuitikia wito wao na kuandaa hafla ya pili Mombasa ili waweze kujadili nyadhifa za kazi huku akiahidi utulivu na nidhamu ya hali ya Juu kuzingatiwa kuliko hapo awali kulipozuka msukosuko wa kugawanyika kwa chama.
Vilevile, amegusia maswala ya "Bipartisan Talks" baina ya serikali na chama pinzani pale ametaja siasa za kenya kuwa za ushabiki na kama mtu alishindwa ingekuwa vizuri akubali ila kwa kuwa chama cha upinzani Ndio wameyataka Hayo Serikali Haina budi Kwenda na mwendo wanaoutaka.
Aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha udiwani wadi ya kipevu -changamwe bwana Emmanuel Amunga,amemzungumzia seneta mteule Miraj Abdillah kama mama shupavu anayewezesha wanawake kupitia miradi yake ya kupeana sodo .Amesisitiza ombi kwa rais aweze kuwateua katika nyadhifa mbali mbali ili pia wapate mgao wao Ili kuwawezesha pia wananchi wa chini waliowapigia kura.
Vilevile,bwana Mohammed Adam alamaarufu (Kipara) ,ambaye aligombea kiti cha udiwani wadi ya old town eneo bunge la mvita, amezidi kutilia mkazo swala la mgao wao haswa kwenye wakati huu Serikali Ipo imara katika mipangilio .
© AKILINYINGI MEDIA
MOMBASA
Kazi safi kaka
ReplyDeleteNakala Safi Kakaa🏁
ReplyDeleteKipara aliwania udiwani Mji wa Kale wala sio Mkomani
ReplyDeleteImerekebishwa
DeleteGood job
ReplyDeletenoma sana 💪
ReplyDeleteKazi nzuri Sana Kijana wetu
ReplyDeleteSafii kijana
ReplyDeleteNice article bro
ReplyDeleteGood work
ReplyDelete🙌🙌💯
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteGood piece
ReplyDeleteGreat work man keep the grind 💯😎🤲
ReplyDeleteKazi nzuri duuh
ReplyDelete