MAQDIS FC NDIO MABINGWA RABAI TALENT CUP
. Picha ya wachezaji wakimenyana. (Maqdis ni Wenye jezi nyeupe na kaptura nyeusi na power ni yenye jezi nyekundu na kaptura ya kijani.)
Maqdis fc wameibuka mabingwa wa fainali ya Rabai Talent cup, baada ya kuinyuka timu ya Power United mabao 3-2 katika uwanja wa Mgalla wadi ya rabai kisurutuni Katika eneo bunge la Rabai Kaunti ya Kilifi.
Michuano hiyo Iliandaliwa na Kamoti Saburi maarufu Kamoti Junior kwa ajili ya kuwaleta vijana pamoja na kuinua vipaji vyao vya soka, timu 32 zilishiriki michuano hiyo.
Kwenye fainali hiyo vijana wa timu ya Maqdis walionyesha ujasiri baada ya kutoka nyuma na kuchukua ubingwa dhidi ya miamba Power United waliotangulia kuliona lango dakika za mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Kamoti ameweza kuwapongeza vijana hao kwa kuonyesha nidhamu na bidii kwenye tasnia hiyo ya soka na kufanya mashabiki kuhemka kwa furaha.
Timu zote zimeweza kupata zawadi mbali mbali ikiwemo vikombe, jezi ,mipira na pesa taslim elfu 20,000.
Aidha fainali hiyo ilichachishwa zaidi baada ya mbunge wa eneo hilo Anthony Kenga Mupe kuwasili na kuweza kuzidi kuwapa motisha wachezaji na vijana kwa jumla.
Mbunge huyo, ameipa talanta kipaumbele na kuahidi kuanzisha michuano itakayo shirikisha timu eneo bunge lote la Rabai Kenga Wehu Super cup itakayo zinduliwa mwishoni mwa jumalijalo.
Kenga aidha amewasihi vijana kutojihusisha na dawa za kulevya na badala yake wajihusishe na michezo akisema kwamba dawa hizo zina athiri nyota zao za maisha ya usoni.
Wakati huo huo ,Kenga amewasihi walimu kutowatuma wanafunzi nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa karo akisema kuwa afisi yake inaweka mikakati ya ufadhili wa elimu ili wanafunzi wapate kusoma bila tashwishi.
Mbunge huyo , ametaja kuwa uhaba wa maji unaoshuhudiwa katika eneobunge hilo na akahakikisha kuwa serikali ya kaunti pamoja na serikali kuu wapo kwenye mchakato ili swala hilo kutatuliwa ipasavyo.
"nitahakikisha serikali ya kitaifa na ile ya kaunti zinalishugulikia kwa haraka tatizo hilo ambalo limekuwa miaka nenda miaka rudi", alisema.
Mwisho.
© AKILINYINGI
MOMBASA



On top💯
ReplyDeleteGreat article 😊👏
ReplyDeleteKazi nzuri sana @inclusive tv
ReplyDelete