EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.
Kiwanda Cha ushonaji Nguo Cha EPZ Changamwe kimewasimamisha kazi zaidi ya wafanyakazi elfu moja bila ilani mwafaka inayotakiwa.
Hili limetokea baada ya wafanyakazi hao kuwa katika mvutano na kampuni hiyo dhidi ya kutosajiliwa katika mkataba mwafaka wa kufanya kazi njia iliyotumika kusimamishwa kazini.
Baadhi ya wafanyakazi wameweza kulalama masaibu yanayowakumba wakiwa kazini hii ni ikiwemo kutopewa uhuru wa kufanya kazi jinsi inavyopaswa pamoja na kufanyishwa kazi mfululizo bila ya mapumziko .
Pia, viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa changamwe Omar Mwinyi wamejihusisha na swala hili kwa minajili ya haki kutendeka kwa wafanyikazi hao kwa njia ya upesi .
Mwakilishi wa wadi ya changamwe Bernard Ogutu amesisitiza Kuwa yuko tayari kwa lolote lile kuhakikisha Kuwa wananchi hawa wanatendewa haki kulingana na katiba pia kuwapa onyo maafisa wa polisi wanaotumika katika shuhuli hii Ili kuwatimua wafanyikazi hawa wanapoandamamia haki zao.
_AKILINYINGI _MEDIA_
MOMBASA_
Big up brother, good work
ReplyDelete