MAPENZI SHIKAMOO VYUONI


Kwenye kumuumba Binadamu Mwenyezi alimpa upendo kama njia moja ya kuchepua mahusiano na kuwaleta karibu viumbe wake.

Kwenye zama za wazee wetu mapenzi yalidhihirishwa kwa njia kuu sana na kubebwa ghali kama hata ilivyoandikwa kwenye bukrata takatifu.wazee wetu wangeweza kuwapenda wapenzi wao penzi la dhati au tuseme lile penzi tunaloliskia la romeo and Juliet.

Enzi hizi za karne ya ishirini na mbili inashangaza sana mapenzi yakiwa  kama silaha ya chuki, kuumizana na hata kutoana roho kwasababu zisizoeleweka .

Tukizamia Kwa umri Wa mabarobaro vijana haswa walioko kwenye vyuo vikuu wamejipata kwenye tabu ya bahari hii ya mateso iitwayo mapenzi.Sijui mimi Akili nyingi labda sifahamu mapenzi ni nini lakini jinsi wengi wanavyobakia hoi inashangaza sana.

Vijana wanaanza kwa kuwa na mazoea kama njia moja ya kufahamiana tu alafu kwa kipindi kifupi kunazuka uhusiano mkubwa Wa mtu kutopata Usingizi asipimuona au kuzungumza na Mwenzake nafkiri tunajua fika mazoea yana tabu.

Ghafla tu kupitia mitandao ya kisasa wapenzi wengi wanapata mpaka fursa za kujianika wazi wazi ili kudhihirisha hadharani fulani ni wangu na mimi ni wake hiki ndo kipindi cha kuwekana moyoni.

Lakini utakubaliani nami ama ukatae kuwa halua hii tamu hugeuka kuwa shubiri kwa mambo tata ama vizingiti ikiwemo ibilisi pesa ,kutotosheleka kimwili, ulafi wa kuwa na watu wengi ama tabia za kiajabu tunazoita ukware.


Hatua kama hii kwa hawa jamaa vyuo vikuu huwapiga chini baada ya mpenzi wa fulani kuona mapenzi ya kina fulani yananawiri kwa labda kutoana mitoko ,sherehe na hata kununuliana "surprise".

Kwenye vichwa vya habari ni mara nyingi tumeskia na Kuona vijana wengi walio jitosa penzini wakijitoa uhai wengine wakiacha kabisa kupenda na Wengine Hata kuhamisha mapenzi yao Kwa jinsia moja walio.kama ni wa kike anabakie kupenda wanawake tu na kama wakiume anaanza kuvutiwa na wanaume wenzake.

Hapa ndipo unapata Wazazi wanasubiria wajukuu Kwa hamu Bahati Mbaya wanapatana na makuu....

Niruhusu niseme hivi,kabla hatujajitosa kwenye ulimwengu huu wa mapenzi ni vizuri tujiandae kupata Ushauri Hata angalau kutoka kwa wazee wetu na kujipanga jinsi ya kukabiliana na vikwazo tunavyopata safarini .
Uamuzi wetu ndio muhimu kwa sana kwenye maisha na tujizatiti Sana tusijotoa suluhu ya Kutoa uhau au kujiunga na mambo hayapendezi jamii.
Nafkiri mtaniwia radhi labda nikiibua kikwazo ila nipe ruhusa nitilie kokomo

#Akili nyingi
#Fikra za Kichawi 

Comments

  1. Kwa hakika maamuzi yetu ni muhimu sana kwa haya maisha

    ReplyDelete
  2. Alhamdullilah kiswahili nayo daah

    ReplyDelete
  3. Creativity 💯💯

    ReplyDelete
  4. Kazi safi✍️🔥🔥

    ReplyDelete
  5. Sadakta kakangu.
    Makala mazuri.
    Hongera na kongole kwa kazi nzuri.

    ReplyDelete
  6. Kiswahili kitukuzwe
    #Akili nyingi

    ReplyDelete
  7. Msingi mkuu wa mahusiano ni mawasiliano ya kumsikiliza na kumuelewa kwanza mwenzako kabla ya wewe kueleweka.

    ReplyDelete
  8. Keziah Ndunge# good job rafiki, i thnk u are good author 😊

    ReplyDelete
  9. Mbele kwema
    @mcsenturians

    ReplyDelete
  10. Ahsante kwa Malala haya mtu na Akili zake Akili nyingi, lakini Kuna jambo kuhusu kutokwa roho kimapenzi na kuingiwa na shetani ya mapenzi ya jinsia Moja, pengine je Kuna utafiti wowote wa kisayansi una dhibitisha Hilo dai lako. Na pia zama za kale kulikua na huu uchafu wote, umalaya, usaliti etc fikra yako kwamba watu wa kale walikua wamenyooka Ina Msingi upi kihistoria.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu wangu Wa Ushauri Bwana Nato Mwenyewe 🙏🙏🙏🙏🙏

      Delete
  11. Hii n true broo . keep up

    ReplyDelete
  12. Boom daad akili nyingi kweli

    ReplyDelete
  13. Kazi safi kaka
    Kiswahili ndo lugha ya mapenzi ❤️💯

    ReplyDelete
  14. nkubali broo noma sna iyo

    ReplyDelete
  15. Mapenzi hayana mwenyewe heri vijana tuulizie mawaidha kabla ya kuingia katika Mapenzi kwa sababu wengi tunajitia kwa shida kwa sababu ya kuingia tu. ..

    ReplyDelete
  16. Kazi nzuriii nduguu

    ReplyDelete
  17. Pongezi bro kazi nzuri

    ReplyDelete
  18. Kazi kuntu...eenyeewe mapenzi kwio😂😂😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenda Zako Kumbe Ndo Maana Ulinikataa🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

      Delete
  19. Ukweli kabisa💯💯

    ReplyDelete
  20. Akili nyingi wewe ni mkweli kabisa bazuu nakutambua

    ReplyDelete
  21. Nice... This is a very good article,, keep it up Mzee😂

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VIJANA KAZINI

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.