MAWINGU YA LAANA

Mara nyingi tunafahamu fika mawingu yakitanda angani huwa ni mvua ipo tayari kunyea ishara ya baraka lakini hili limegeuka kinaya!.
kwa zaidi ya misimu minne ardhi yetu imekuwa ikishuhudia kiangazi kikali kisichodhibitika kwa hali ya kushangaza au labda tuseme mkosi mbaya .
    picha kwa hisani ya gazeti la star


Kulingana na utafiti wa wanasayansi limetajwa swala la kuchafuka kwa anga kwa mambo tunayoyafanya sisi binadamu ikiwemo utumizi wa kemikali sumu,ukataji miti na uchafuzi wa mazingira na mengineo mambo yanayosababisha kuvuja kwa miale mikali ya jua inayopasua ardhi na kuiacha nchi kavu.
.    Picha kwa hisani ya gazeti la star 

Hapa nchini zipo sehemu zenye hatari hii kubwa ikiwemo ; Garissa, Isiolo, Kajiado, Kitui, Mandera, Marsabit, Laikipia, Samburu, Tana River, Turkana, na wajir
.    Picha kwa hisani ya gazeti la star 


 Utafiti umebaini kuwa zaidi ya raia milioni nne nukta moja wanaoishi kwenye sehemu hizi wamehadhirika pakubwa na janga hili lA ukame ikiwemo ukosa mlo ,Maji ya uhai  na hata mifugo yao kudhoofika kukosa dhamani na kufariki swala linalotikisa taifa nzima kwa Sasa .Hivi umewahi kuskia ng'ombe akishuka bei mpaka kiasi cha kuuzwa Shilingi mia tano?, msomaji wangu nafahamu kuwa hili halikuingii akilini lakini hapa ndipo hali imefikia sijui niseme labda ni nuksi kwenye maisha au nikipigo kutoka kwa Maulana...? Aiseee,Akili nyingi nawaza na kusikitika.
.     Picha Kwa hisani ya Facebook 

Mzigo wa kupanda kwa  gharama ya maisha ukiwa begani ukame nao unatupa micharazo kwa kupungua kwa mazao ya shambani tunayotegemea kama nchi huku mvua ikisusia kunyesha kama inayotarajiwa ! ,ni swala tata .

Serikali imechukulia pakubwa jukumu hili zito kuhakikisha angalau raia wanapata ukombozi kutoka kwenye lindi hili baada ya mtukufu rais wa jamuhuri ya kenya William Ruto pamoja na mashirika mengine kuanza shughli ya kusambaza shehena ya chakula cha msaada kwenye sehemu zilizoathirika ili kuleta afueni heko.

     Picha Kwa hisani ya kbc

Najua msomaji wangu mpendwa upo kwenye taharuki kwa hili lakini mimi Akili nyingi ningependa tusaidiane kwa kubuni njia mbadala za kupambana na jinamizi hili.Ndio upo mradi umetolewa na serikali wa maswala ya upanzi wa miti zaidi ya bilioni moja kwa kipindi fulani lakini mbona tusubirie amri na ilhali ni Jukumu letu kushirikiana kutenda hili...?

Je,Unafikiria ni mbinu hii pekee inayoitajika..? Nafkiri kazi ipo.

Kabla sijamwaga wino ningeomba walio na imani wazidi kutia  dua kwasana ili angalau Subaha Ntrehemezi atuwezeshe na atunyeshee mvua ya mavuno ili kudhibiti njaa na ukame.
jambo hili ni letu sote na pamoja tutadhibiti ukame.

#Fikra za Kichawi
#Akili nyingi
#Mombasa

Comments

  1. Such a great publishment there looking forward to seeing you do much better than this... Congratulations

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri. Mola akuzidishie maarifa, hekima na nguvu unazohitaji katika kazi yako.

    ReplyDelete
  3. πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  4. Sadakta kakangu. Makala haya yanapendeza. Heko, hongera na kongole kinara! πŸ‘πŸ‘

    ReplyDelete
  5. Nice article πŸ₯°

    ReplyDelete
  6. This is an art of education... With this kind of work I'm sure we know where we are heading as a nation

    #Akilinyingiblogspot

    ReplyDelete
  7. Legit article 😊😊

    ReplyDelete
  8. Inagusa moyo sana nakala Safi hii

    ReplyDelete
  9. Keep up the work...πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  10. Article Iko fiti nduguu ✊

    ReplyDelete
  11. The article is awesome… but it’s a sad story for kenya

    ReplyDelete
  12. Kweli fikira za kichawi hizi...Kazi safi🀝🀝

    ReplyDelete
  13. Umeyasuka makala haya yakasukika kwa kuoanisha fani na maudhui kwa umahiri wa aina yake.Heko na hongera kakangu.

    ReplyDelete
  14. Continue with the same spirit my friend 😊😊

    ReplyDelete
  15. Kazi safi,,,,mola akuzidishie hekima

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VIJANA KAZINI

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.