VIJANA KAZINI

.   Picha ya vijana mombasa

Je, vijana ni kina Nani...? ,wengi huwazungumzia  kwa kauli bora ya  uongozi wa kesho wenye maarifa na Nguvu zaidi kwenye milki ya majukumu mazito Sio tu ya familia bali ya jamii nzima. 

Kwa kipindi cha muda mrefu hapa nchini wimbo wa ukosefu wa ajira umekuwa kama kibwagizo kila kuchao huku maelfu ya wanafunzi wanaohitimu vyuoni wakibanana mjini kila mmoja akiwa na lengo la kufanikisha maisha.

Licha ya msururu huu wa neno "Sina Kazi " kusambaza kwa kasi, vijana wameweza kufunguka macho na kuona ya mbeleni huku wakizamia kwenye mitandao ili kukwachua vibarua vya peni kadhaa kwa kimombo tunaziita "online jobs". 

.   Picha kwa hisani ya Ajira

Wengine wamejitosa kwenye mashirika kadhaa yanayotoa mafunzo ya kiufundi, ufadhili wa miradi na biashara aidhaa kwa vikundi au mtu binafsi maswala yanayompa kijana uwanja wa kujiendeleza.
.   picha kwa hisani ya shirika la Swahili            pot 


Serikali ipo kwenye mapambano Angalau kufungua njia mbadala kukabili janga hili la ukosefu wa ajira hii ikiwemo kutoa mikopo murua na inayokatwa ada ya chini kiasi cha kuweza kumudu kila mmoja Katika vitengo tofauti fursa inayompa kijana Mwanga Wa kupasua Maisha kwenye uwanja wa biashara.

.    picha kwa hisani ya facebook 

Bidii hii yote pande zote mbili ni ishara tosha kuwa miaka ijayo wengi watakuwa wameweza kujiajiri na maisha kuwa kwenye ngazi ya kisawa ni jukumu la kila mmoja kuwa mpambanaji bora ili kuweza kuyafulia maisha dafu

Nina lengo na tumaini kubwa kuwa vijana wanaweza na wataweza kuibia ubunifu zaidi haswa kwenye sekta za biashara,sanaa na hata mawazo yanyopania kusonga mbele .

#fikrazakichawi.
#Akilinyingi.
#Mombasa

Comments

  1. Makali Safi sana kwa vijana

    ReplyDelete
  2. Nakala Safi sana kwa vijana

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri Yohana keep it up

    ReplyDelete
  4. Makala mazuri. Kazi safi kabisa. Hongera kaka!

    ReplyDelete
  5. The young generation simply needs to renew, refresh and maintain the current status of society.

    ReplyDelete
  6. Great keep it burning 🔥 more fire

    ReplyDelete
  7. Dope manzee keep it up

    ReplyDelete
  8. Kazi safi big up bro👍

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

POLISI WANASA BANGI CHANGAMWE

EPZ CHANGAMWE YAFUTA WAFANYIKAZI GHAFLA.